MAMBO YAENDA VIZURI SAKATA LA TRA,TFF

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA)  na wizara ya Habari utamaduni vijana na michezo wamekutana kwa ajili ya kujadili suala la TRA kuzifungia kaunti za Ligi za Shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Osiah amesema leo kwamba, baada ya kikao cha pande hizo kila upande umekubalina baadhi ya mambo ambapo anaamini mambo yatakwenda vema hivi karibuni.
Hivi karibuni TRA ilizifunga akaunti hiyo kwa madai ya TFF kudaiwa makato ya zaidi ya sh.mil 157 kutoka kwa mishahara ya makocha wa timu za Taifa kuanzia enzi za Mbrazil MArcio Maximo.