KAMANDA POLISI TANGA ATHIBITISHA KIFO CHA SHARO MILIONEA

Msanii maarufu wa Luninga, Sharo Milionea (pichani), amefariki dunia leo katiak ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga. Kamanda wa Polisi Tanga, Constantine Massawe, amethibitisha kutokea kifo cha msanii huyo aliyekuwa anaimba muziki wa kizazi kipya pia. Habari zaidi zitafuatia.


NIYONZIMA AING'ARISHA RWANDA KAMPALA

Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima (katikati) akidhibitiwa na wachezaji wa Malawi, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda usiku huu. Rwanda ilishinda 2-0, mabao ya Jean Baptiste Mugiraneza dakika ya 37 na Haruna Niyonzima dakika ya 79.

Wachezaji wa Rwanda wakishangilia bao lao la kwanza ushindi.


ZANZIBAR YAANZA KWA SARE TASA TUSKER CHALLENGE 2012

Kiungo wa Zanzibar, Khamis Mcha ‘Vialli’, (kulia) akigombea mpira na beki wa Eritrea, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole jioni hii. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.


Beki wa Zanzibar, Nassor Masoud ‘Chollo’, (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Eritrea, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole jioni hii. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.