BAADA YA COASTAL KUMKANA NYOSO SASA KUPELEKWA AZAM FC

BAADA ya Coastal Union kuigomea Simba kumpeleka wake Juma Nyoso, Simba imeamua kurudi kwa maswahiba wao, Azam Fc ambapo sasa itabadilishana nyota huyo na Aggrey Moris, imefahamika.
Nyoso  pamoja  Haruna Moshi 'Boban'  kwa sasa wanatumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muida usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu, huku beki akipewa pia adhabu ya kushushwa hadi timu B.
Hata hivyo, mchezaji huyo amepinga kushushwa daraja na kutaka kuvunja mkataba wake Simba ambayo hata hivyo imeonekana kumkomalia.
Kiongozi mmoja wa Simba amesema kwamba tayari mazungumzo baina ya Simba na Azam Fc juu ya suala hilo.
Nyoso atakuwa mchezaji wa pili kuwemo katika mpango huo ambapo tayari Simba ipo katika mchakato wa kumpeleka Azam Uhuru Seleman na kumchukua George Owino