YANGA:KIKUBWA NI POINTI TATU SI MAGOLI 6-0 AU ZAIDI KESHO...


KLABU ya Yanga kupitia kwa katibu wake Mkuu, Lawrance Mwalusako imesema imejipanga vema kuhakisha wanashinda mchezo huo na kupata pointi tatu. 
“Kikubwa ni pointi tatu na wala si mabao 6-0 na kuendelea hata tukishinda bao 1-0 ni ushindi tu ambao utatupatia pointi”, alisema 
Mwalusako aliongeza kwamba kikosi cha timu hiyo kilichopiga kambi kwenye hoteli ya kimataifa ya Double Tree By Hilton iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam kipo katika hali nzuri na pamoja na mazoezi wachezaji wamejengwa vema kisaikolojia. 
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani , huku  watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu watalipa sh. 7,000 , wakati watakaokaa  viti vya rangi ya chungwa watalipa Sh. 10,000 , huku  VIP C itakuwa sh. 15,000, VIP B watalipa  sh. 20,000 na VIP A watalipa sh. 30,000.