YANGA YAIFUMUA AFRICAN LYON 3-1

MABINGWA wa kombe la Kagame Yanga, wameendelea kufanya vema katika ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya jana kuifumua African Lyon mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliorushwa 'Live' na kituo cha Televisheni cha SuperSport, mabao ya Yanga yalifungwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' pamoja na Nizar Khalfan aliyepachika mawili, huku lile la Lyon likipachikwana Benedict Mwamlangala.