Skip to main content

YANGA, SIMBA WAINGIZA MIL 390/-


Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000. 
Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49. 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000. 
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22. 
Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.
 Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments