YANGA, KAGERA SUGAR HAPATOSHI KAITABA LEO


MABINGWA wa Soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga leo wanatarajia kushuka katika dimba Kaitaba mjini Bukoba kukwaana na wenyeji Kagera Sugar, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Katibu mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kikosi cha timu hiyo kipo tayari kwa mchezo huo na anauhakika kitafanya vema kwa kuondoka na pointi tatu muhimu.