WAREMBO MISS TANZANIA 2012 WAZURU MLIMA KILIMANJARO

Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakiwa katika picha ya pamoja Oktoba 7, 2012 wakati warembo hao walipo tembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuopata maelezo na kuzungumza na watalii na wapanda mlima huo. Warembo 29 na viongozi wa  Kamati ya Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani.

Mbali na kutembelea hifadhi hiyo lakini warembo hao walishiriki katika tamasha la michezo kwaajili ya kuchangia fedha na vitu mbalimbali kwa watoto Yatima mjini Arusha.

Oktoba 8 warembo wanaendelea na ziara yao ikiwa ni pamoja na kutembelea kituo cha Redio cha RADIO 5 cha mjini Arusha.
 Washiriki wa Redds Miss tanzania 2012 wakiwa katiak picha tofauti tofauti wakati wakiwa katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro KINAPA.
  Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanao panda mlima Kilimanjaro.
 baadhi ya warembo wakipiga picha na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania
  Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanao panda mlima Kilimanjaro.
 Warembo wakiwa wakiwa katika eneo la maegesho ya magari KINAPA
 Wakielekea eneo la kupata taarifa mbalimbali za Mlima Kilimanajaro
 Wakipiga picha na baadhi ya watalii waliowakuta hapo.
 Warembo wa Redds Miss Tanzania wakimsikiliza Afisa Mhifadhi wa KINAPA, Eva Malya aliyekuwa akiwapa taarifa mbalimbali juu ya mlima huo.
 Warembo wakiwa na nyuso za furaha wakiendelea kupata maelezo juu ya mlima
Hapa sasa walibeba mabegi ili wapande Mlima. 
Endelea kutembelea Father Kidevu Blog na ukurasa wa 
http://facebook.com/ReddsMissTanzania2012

Comments