WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA MAKONGO, ST. MARYS NA MAMA SALMA KIKWETE WASHUHUDIA SARAKASI ZA TIGO MAMA AFRIKA

Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliohudhuria onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika lililodhaminiwa na Tigo katika Viwanja vya New World Cinema, Mwenge, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Makongo, John Ngowi. Wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule za sekondari za Makongo, St. Mary na Mama Salma Kikwete walihudhuria onyesho hilo.  Ofisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro (kushoto) akishakana mikono na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makongo, Kapteni Mstaafu, Hamisi Mfaume kabla ya onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika kuanza. Katikati ni Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi.   Baadhi ya wanafunzi wa sekondari wakipewa viburudisho kabla ya onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika kuanza.   Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika, wakitoa burudani.   Burudani ikinoga katika onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika.
 Moja ya mchezo ambao uliwavutia wanafunzi wa kurusha matairi meza kwenda meza onyesho la Tigo Sarakasi Mama Afrika.
 Bendi ya Inafrika ikitoa burudani ndani ya onyesho la Tigo Sarakasi Mama Afrika.
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakishindana kucheza baada ya kumalizika kwa onyesho hilo.
Washindi wa kucheza katika shamra shamra za Tigo Mama Afrika, wanafunzi wa Makongo wakipewa zawadi.
 
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika wakishangilia wakati wasanii wa kikundi hicho wakionyesha umahiri wao katika onyesho lililodhaminiwa na Tigo katika Viwanja vya New World Cinema, Mwenge, Dar es Salaam. Zaidi ya wanafunzi 1000 kutoka shule za sekondari za Makongo, St Mary na Mama Salma Kikwete walihudhuria.

Comments