SIMBA YAIKANA YANGA SUALA LA MAPATO


Simba imepigana na mahasimu wao Yanga kuhusiana na mgao wa mil 93 katika mechi yao na kusema wanakubaliana na mgao huo waliopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga jana kupitia kwa Katibu wake , Lawrance Mwalusako iliitaka TFF kuchunguza tatizo la kupatikana kwa mapato kiduchu ya mil 390,568,000 yaliyotokana na watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. 
Mwalusako alisema idadi ya watazamaji 58,000 iliyotolewa na TFF  ilikinzana na ile ya SuperSport kwa makadirio ya chini tu iwapo kila mtazamaji aliyeingia uwanjani humo angelipa walau sh 15 000 tu zingepatikana zaidi y ash milioni 6,000. 
Hata hivyo, Simba kupitia kwa msemaji wake Ezekiel Kamwaga,imesema haijafanya utafiti juu ya suala hilo, huku ikiangalia zaidi namna ya kudhibiti mapato yatokayo na mechi zao.