SIMBA YAFANYA KWELI VPL


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba ‘Wekundu wa Msimba’ wamezidi  kuendeleza kampeni za kutetea taji lao baada ya kuwatoa nishai  maafande wa JKT Oljoro kwa  mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo mabao ya Simba yalifungwa na Amri Kiemba aliyefunga mawili, huku Emmanuel Okwi na Felix Sunzu kila mmoja akipachika moja.
Bao la kufutia machozi la Oljoro lilipachikwa na Paul Nonga.