SIMBA SC YAWAFUATA 'WAGOSI WA KAYA'

MABINGWA wa ligi kuu Bara Simba Sc wanaondoka jijini Dar es Salaaam leo kwenda Tanga tayari kwa mchezo wao dhidi ya wenyeji Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' utakaopigwa jumamosi katika dimba la Mkwawani.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba kikosi cha timu hiyo ambacho baada ya mapumziko ya siku mbili jana kilifanya mazoezi katika uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Alisema wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokuwa Haruna Shamte ambaye bado ni majeruhi.
Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa  na pointi 16.