SHINDANO LA UNIQUE MODEL 2012 LAZINDULIWAMkurugenzi wa Unique Entertainment, Methuselah Magese (kati) akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya holiday Inn jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa shindano la Mitindo 'Unique Model 2012' ambapo usaili utafanyika Novemba 18 katika ukumbi wa Lamada Hotel iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, huku fainali za shindano hilo zitafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba.
Kushoto ni mkuu wa kitengo cha fedha, Happy Mushi na kushoto ni mkuu wa Itifaki, Mariam Hamis.