PUNGUZA "STRESS" ZA WIKI NZIMA NA SKYLIGHT BAND KILA IJUMAA THAI VILLAGE MASAKI JIJINI DAR.


Baadhi ya Wanamuziki wa SKYLIGHT BAND wakishambulia Jukwaa mwishoni mwa wiki katika show ya kukata na shoka kwenye kiota chenye upepo mwanana cha THAI VILLAGE Masaki jijini Dar es Salaam. Pichani ni Rappa Sam Machozi akisindikizwa na Wenzake Aneth Kushaba AK 47 pamoja na SONY MASAMBA.

Sam Machozi kazini. Hapa unapata kila kitu Style zote za muziki kuanzia Dancehall, Reggae, R & B, Azonto na nyinginezo bila kusahau Kwaito.

Mdogo mdogo wapenzi wa Skylight Band wakaanza kujimwaga kwenye dancing floor.
Uzao wa Bongo Star Search binti mwenye kipaji na sauti nyororo Mary Lukas.
Vijana machachari wadogo wakifanya mambo makubwa.
Joniko Flower, Aneth Kushaba AK 47 sambamba na SONY MASAMBA.
Tumba zikikung'utwa kisawa sawa.
Hawa ndio Malkia wa Skylight Band wenye sauti za kumtoa nyoka pangoni. Kushoto ni Mary Lukas sambamba na Meneja wa Band Aneth Kushaba AK 47 wakiwajibika.
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali.
Taratibu dancing floor ikiendelea kupendeza.
Sam Machozi sambamba na marapa wenzake.
Hapa ni kikongo kimelala anaitwa SONY MASAMBA.
Joniko Flower akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
Hapo sasa hakai chini mtu... Sebene limekolea tena..... Usipime babuuu..... ni Kila Ijumaa katika Ukumbi wa THAI VILLAGE Masaki jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu usiku ndio mahali pa kupunguza msongo wa mawazo ya wiki nzima.
Wadau wa Skylight Band na nyuso za furaha.
Usipime Babu........ SKYLIGHT BAND moto chini wewe.
Wadau wa SKYLIGHT BAND walikuwepo ndani ya nyumba.
Bila kusahau nyama choma zinapatikana pia.