OKWI,KEITA NA REDONDO KUIKOSA CAOSTAL UNION JUMAMOSI


Okwi

MABINGWA wa ligi kuu Bara, Simba wameondoka mchana wa leo kwenda mjini Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi hiyo dhidi ya wenyeji Coastal Jumamosi katika dimba la Mkwawani mjini humo.
Hata hivyo, Simba imeondoka bila ya nyota wake Emmanuel Okwi na Ramadhan Chombo 'Redondo', HAruna Shamte na Komabil Keita.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba Okwi amekwenda kwao Uganda kwa ajili ya kuichezea timu ya Taifa 'The Cranes' ambayo ipo katia kampeni za kuwania kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.
 Alisema Keita naye ameachwa kutokana na kuwa na maumivu ya taaya, sambamba na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ambaye ana malaria.
 “pia katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 22 na viongozi watano hatokuwemo kipa Waziri Hamadi, Omari Seseme na Haruna Shamte ambaye ni amjeruhi,”alisema.