NGASSA, KIGGI NAO KUIKOSA COASTAL UNIONMUDA mfupi kabla ya kikosi cha Simba kuondoka mchana wa leo kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu Bara dhidi ya wenyeji Coastal, idadi ya wachezaji watakaokosa mchezo huo imeongezeka baada ya mshambulijia wa timu hiyo Mrisho Ngasa.
Awali, ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema Ngasa ambaye alikuwa na Malaria amepona na atakuwwemo katika safari ya Tanga lakini baada ya daktari wa timu hiyo kuwafanyia vipimo wachezaji kabla ya kuondoka ilibainika kwamba Ngasa bado ni mgonjwa.
Kamwaga alisema mbali na Ngasa, majeruhi mwingine ni Kigi Makasi ambaye ataungana na haruna Shamte na Komabil Keita .
Aidha, katika msafara huo pia hatokuwemo mshambuliaji wao Emmanuel Okwi ambaye amekwenda kwao Uganda kujiunga na timu ya Taifa, huku Abdala Seseme na Waziri Mahadi wakiachwa kwa sababu za kiufundi.Makipa

Juma Kaseja, Wilbert Mweta

Walinzi

Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema.

VIUNGO

Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban

Washambuliaji

Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma

Ambao hawakwenda'

Ngassa, Redondo..................Malaria
Haruna Shamte..................Enka
Kiggi Makassi..................Goti
Okwi...............Kuitwa timu ya taifa
Abdallah Seseme, Wazir Hamad,