MILOVAN AMPA MAJUKUMU MAZITO KAPOMBE


Milovan Cirkovic, kocha mkuu wa Simba
Kocha mkuu wa  Simba Milovan Cirkovic, amemkabidhi majukumu beki wake Shomari Kapombe ili kuhakikisha anakula sahani moja na mshambuliaji  wa Yanga Saidi Bahanuzi katika mechi ya kesho ya ligi kuu ya Vodacom baina ya timu hizo kwenye dimba la Taifa.

Milovan alisema amempa majukumu hayo Kapombe kutokana na aina ya uchezaji anaocheza hasa wa kutumia akili pamoja na nguvu na haswa ikizingatiwa kuwa  anajua namna ya kukaba na ni mwenye kujua nini anafanya ili asilete madhara langoni mwake anapokuwa uwanjani kwa muda wote wa mchezo.

Mserbia huyo alisema anaamini Bahanuzi ni mmoja wa washambuliaji mahiri na wenye kutumia akili na nguvu hivyo kutomuwekea ulinzi imara anaweza kufanya kitu mbaya kwa timu yao.

“Namuamini Kapombe na anaweza kuwa mtu muhimu katika ulinzi katika mechi ya keshokutwa hivyo wanasimba wanahitaji kumpa msaada kwa muda wote wa mchezo.

Aidha kocha huyo amewataka wana Simba kuwa watulivu kwanai ana uhakika wa kushinda katika mechi hiyo kutokana na maandalizi ya uhakika aliyofanya.