KASEJA, NGASA, KAPOMBE NA KAZIMOTO WAULA


WACHEZAJI wanne wa mabingwa wa ligi kuu Bara, Simba wakiwemo  Nahodha Juma Kaseja, Mrisho Ngasa, Shomari Kapombe na Mwinyi Kazimoto wanatarajiwa kuonekana katika nchi mbalimbali duniani baada ya wasifu wao na baadhi ya picha cha michezo yao kurekodiwa kabla ya kurushwa na kituo cha Televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
 Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameiambia Sports Lady blog kwamba, isema zoezi hilo limewezeshwa na wadhamini wa timu hiyo kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro na kuongeza kuwa ni hatua nzuri ya kuelekea mafanikio ya kupata timu za kucheza nje ya nchi kwa wachezaji hao. 
kama mjuavyo SuperSport inaonekana duniani kote hivyo wachezaji wetu watapa kuonekana na vilabu mbalimbali na kwa njia hiyo wanaweza kupata timu za kucheza katika sehemu tofauti duniani,”alisema