FILBERT BAYI AULA CCM


KATIBU Mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi amefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki mkutano mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwakilisha Wilaya ya Karatu. 
Bayi amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni baada ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley(545), Ori Pembe (460), Fabiola Deo (456) na Amsi aliyepata kura 322.

Katika uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo aliyepata kura 512 na hivyo kumwangusha  Gerald Gwaha aliyepata kura 148  huku mgombea mwingine aliyefahamika kwa jina la Tippe alijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa nafasi kamati kuu ya halmashauri kuu (NEC)Awaki Tlemai alishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 545 na Daniel Ilakwahhi aliyekuwa wa pili kwa kupata kura 114.

Comments