BOBAN AMUWEKA WIKI MBILI NJE YONDAN

BEKI wa Yanga Kelvin Yondan atalazimika kukaa nje ya dimba kwa wiki mbili ili kujitibu mfupa wa goti alioumizwa na kiungo  wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' katika pambano la timu hizo lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Yanga, Juma Sufian amesema kwamba baada ya kufanyiwa uchunguzi, Yondan alionekana kupasuka mfupa uitwao kitaalam Fibula, na hivyo kupona kwake itachukua wiki mbili.