TWITE, YONDAN WAIDHINISHWA YANGAHATIMAYE kamati  ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF imewaidhinisha kuichezea  Yanga  mabeki  Mbuyu Twite na Kevin Yondan ambao waliwekewa pingamizi na mahasimu wao nchini, Simba .
Katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi jana, pamoja na maamuzi hayo Yanga wametakiwa kuilipa Simba dola  32,000 ambazo walimpa  Twite ili ajiunge nao kabla ya Yanga kuingilia kati na kumsajili.