TIP TOP CONNECTION WAKAMILISHA VIDEO YA 'RIZIKI'


KUNDI la Muziki wa kizazi kipya la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam limekamilisha kurekodi video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Riziki’
Meneja wa kundi hilo Hamis Tale ‘Babu Tale’ ameiambia Dina Blog kwamba lisema jana kazi ya kurekodi video hiyo imefanywa na kampuni ya Apex huku upigaji picha ukifanywa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, sasa linafanyika zoezi la kuihariri video hiyo ambapo kama mambo yakienda vizuri wataiachia hewani wiki ijayo.