SIMBA WALEEEEEEE, YANGA MNALO

Sunzu akimpongeza Edward na Kiemba baada ya kufunga bao la ushindi


Na Mahmoud Zubeiry
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza mabao 2-1 Ruvu Shooting ya Pwani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake mshambuliaji chipukizi, Christopher Edward aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 80 na kuifanya Simba ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu, nyavu zake zikitikiswa kwa mara ya kwanza leo.
Simba sasa inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi saba, wakati watani wao wa jadi, Yanga wana pointi nne tu baada ya mechi tatu.   
Hadi mapumziko, Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya 29, akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’.
Katika dakika ya 45, kipa Benjamin Haule wa Ruvu Shooting alipangua mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Daniel Akuffor baada ya beki mmoja wa timu hiyo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili, Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha maarufu nchnini, Charles Boniface Mkwasa ilisawazisha bao dakika ya 80, baada ya Seif Rashid kutumia vizuri makosa ya beki Juma Nyosso dakika ya 75.
Seif aliupitia mpira miguuni mwa Nyosso, ambaye alianzishiwa na kipa Juma Kaseja na kutokana na kuchelewa kuamua, akasababisha kilichotokea.
Shukrani wake, chipukizi Edward aliyeifungia bao la ushindi Simba inayofundishwa na Mserbia, Milovan Cirkovick dakika ya 80.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Juma Nyosso, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Edward, Felix Sunzu, Daniel Akuffo/Boban na Mrisho Ngassa.
Ruvu Shooting; Benjamin Haule, Michael Pius, Mau Bofu, George Michael, Said Suzan, Gideon David, Abdulrahman Mussa, Hassan Dilunga, Paul Ndauka/Seif rashid, Hussein Said na Said Dilunga. 

Comments