SIMBA SC WE ACHA TU, YAILAZA PRISONS 2-1

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanbzania Bara Simba wameendelea kukalia kiti cha ligi hiyo baada ya leo kuibanjua Tanzania Prisons mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Katia mchezo huo Prisons ilianza kuandika bao katika dakika ya sita kupitia kwa nyota wake, Lugano Mwangama, kabla ya Felix Sunzu kusawazisha katika dakika ya 45.
Mrisha Ngasa ndiye alipeleka ushindi huo Msimbazi baada ya kufunga katika dakika ya 56 na hivvyo kuifanya Simba kufikisha pointi 12,huku Azam wenye pointi 10 wakishhuka hadi nafasi ya pili.