SIMBA RAHAAA...YATWAA NGAO YA JAMII

MABINGWA wa ligi kuu Bara Simba, wametwaa ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam Fc mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo,Azam Fc ilianza kwa kufunga maabao yake kupitia kwa John Bocco 'Adeboyor' na Kipre Tchetche kabla ya Simba kujipanga na kurudiskupitia kwa Daniel Akuffo, Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.