SERENGETI BOYS KUIVAA ASHANTI UNITED UWANJA WA KARUME LEO


TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) baada ya ziara ya Mbeya imerejea Dar es Salaam ambapo inaendelea na maandalizi na leo inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya daraja la kwanza ya Ashanti United.
 
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kwa kiingilio cha sh. 500 tu.