PAZIA LIGI KUU ZANZIBAR LAFUNGULIWA


 Beki wa timu ya Mafunzo Ali Othman (kushoto) akiokoa hatari galini kwake mbele ya mshambuliaji wa timu ya KMKM Tizzo Charles, katika mchezo wa ufunguzi wa ligi Kuu ya Grand Malt uliofanyika katika uwanja wa amaan timu ya Mafunzo imeshinda 1--0.

 Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo Jaku Joma (kulia )  akichuwana na mlinzi wa timu ya KMKM  Khamis Ali, katika mchezo wa ligi Kuu ya Grand Malta uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Mafunzo imeshinda 


Na Ally Mohammed, Zanzibar
Pazia la ligi kuu Zanzibar limefunguliwa jana  kwa mechi mbili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti, kwenye uwanja wa Amaan kisiwani Unguja Mabaharia wa KMKM walikutana na Mafunzo, ambapo mechi hiyo imemalizika kwa Mafunzo kuchomoza na ushindi wa bao 1-0, bao la mafunzo likipatikana katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza kupitia Mohammed Abdulrahman. Huko kisiwani Pemba nako kilipigwa mechi moja ikiwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Super Falcon na Chipukizi ambapo kwa mara nyengine tena Super Falcon ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kimataifa ( LIGI YA MABINGWA AFRIKA) wamezidi kuonesha udhaifu baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa bila kutoka kwa Chipukizi, hii ni mechi ya sita mfululizo Super Falcon wanaendelea kupokea kipigo, wakianzia katika michuano ya BancABC Super 8, ambapo walipoteza mechi zao zote 3 za hatua ya makundi, kabla ya kukubali kipigo cha 3-1 kutoka kwa Jamhuri katika mechi ya ngao ya Jamii iliyochezwa Septemba 1 mwaka huu katika uwanja wa Amaan, juzi wakicheza na Coastal Union ya jijini Tanga katika mechi ya kirafiki, mchezo uliochezwa uwanja wa Ngome, Fuoni, Wilaya ya Magharibi, Unguja walifungwa 2-0.

Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi mbili, katika uwanja wa Amaan kisiwani unguja, Klabu ya Malindi ambao wamenunua daraja kutoka kwa Miembeni SC watacheza na timu iliyopanda daraja msimu huu Bandari na katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba washindi wa pili wa ligi iliyopita, Jamhuri wakicheza na Duma, mechi zota zinatarajiwa kuanza saa 10:30 jioni.

Ligi kuu ya Zanzibar, ambayo msimu huu inafahamika kwa jina la Zanzibar Grand Malt Premier League kutokana na mdhamini kinywaji cha Grand Malt, inashirikisha timu 12, huku timu 8 zikitoka kisiwani Unguja na timu 4 zikitoka kisiwani Pemba, timu zinazotoka kisiwani Unguja ni  Bandari, Chuoni, KMKM, Mafunzo, Malindi, Mundu ambao wamenunua daraja kutoka kwa Miembeni United, Mtende iliyopanda daraja msimu huu na Zimamoto.

Kwa upande wa kisiwani Pemba ni Chipukizi, Duma, Jamhuri na Mabinwa watetezi, Super Falcon.

Comments