OKWI AWATULIZA SIMBA, KUONGOZA MASHABMULIZI DHIDI YA AZAM FC J'4


KIKOSI cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba kimezidi kuimarika baada ya mshambuliaji wake wa Kimataifa, Emmanuel Okwi kurejea jioni ya leo  na anatarajiwa kuungana na wenzake katika mazoezi yanayoendelea kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe.
Okwi alikuwa akiitumikia timu yake ya Taifa ‘The Cranes’ ambayo jana ilicheza mechi ya  kuwania nafasi 15 za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani na kufungwa bao 1-0 anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba watakoshuka katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam keshokutwa kukipiga na Azam Fc katika mchezo maalum wa kuwania Ngao ya jamii (Community Shield). 
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba ujio wa Okwi makali ya timu hiyo katika mchezo wao na Azam kesho pamoja na ligi kuu kwa ujumla inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15.
Alisema kikosi cha Simba kipo katika hali nzuri kikiendelea na maandalizi yake ya mchezo huo huku  pia mshambuaji wake mwingine wa kimataifa Mzambia Felix Sunzu aliyekwenda kumzika dada yake Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) akitarajiwa kuwasili leo.