MISS TABATA ATWAA UMALKIA WA ILALA


Na Mwandishi Wetu
Miss Tabata Noela Michael (18) usiku wa kuamkia leo aliibuka mshindi taji la Redds Miss Ilala 2012 katika shindano iliyofanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni.
Noela ambaye anajiandaa kuingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza kidato cha sita, aling’ara katika usiku huo ambao alipata upinzani mkali kutoka kwa Magdalena Roy Munisi (21) wa Dar City Centre aliyeshika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mary Chizi wa  Ukonga.
Kwa kutwaa umalika huo Noela amejishindia Sh. Milioni 1.5 wakati Magdelena amepata Sh Milioni 1.2 na mshindi wa tatu, Mary amepata Sh. 700,000.
Warembo wote watatu wataiwakilisha  kanda ya Ilala katika shindano la Redds Miss Tanzania litakalofanyika baadae mwaka huu jijini Dar es Salaam.