Skip to main content

MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA – SEHEMU YA PILI


Na Onesmo Ngowi
 
             Masumbiwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa endelea………………………………….!

             Kuanzia karne ya 16 matukio mbalimbali yaliyotokea katika bara la Ulaya na Mashariki ya mbali yalichochea ustaarabu uliopelekea mambo mengi kubadilika. Mabadiliko haya ni pamoja na watu walivyokuwa wanachukuliwa na kuthaminiwa. 


              Dola mbalimbali kubwa kama Mongolia, Manchuria, Ujapan, Urumi, Uyunani, Ottoman n.k zilikuwa kama zimekufa au kupungua nguvu kiasi cha kuruhusu mabadiliko hayo. Ustaarabu huu ulishinikizwa haswa na mabadiliko ambayo dunia ilikuwa inapitia. Wanadamu walianza kuwa na mwelekeo tofauti kabisa katika kuyajali maisha yao.

                Pengine ni katika Mitholojia ya Kigiriki (Greek Mythology) ambapo ushujaa ulipoelezwa kwa ufafanuzi zaidi. Kwenye Mitholojia ya Kigiriki neno Shujaa au Bingwa (Hero) limeelezwa kama “Mwanamke au mwanamme wa ushupavu na nguvu kubwa anayeheshimika kwa mafanikio yake” 

               Mitholojia ya Kigiriki inatuelezea mashujaa wa aina mbalimbali kama vile Hercules, Perseus, Theseus, Odysseus, Bellerophon na Atlas. Wengi wa mashujaa hawa kwenye Mitholojia ya Kigiriki walijijengea sifa kubwa sana kwenye jamii na wengine walifananishwa na baadhi ya miungu yao.

               Ugiriki pia ilitoa mashujaa wengine mbalimbali kama vile Alexander the Greatj ambaye alikuwa ni Jemadari na shujaa wa vita aliewahi kuwa Jemadari mdogo kuliko wote duniani na kuweza kueneza dola ya Kiyunani toka ukanda wa bahari ya Mediterania hadi Afrika ya Kaskazini. 


                Aidha ni huko huko Uyunani ambako mashujaa wakubwa wanafalsafa kama kina Soctates, Plato na Aristotle walisheheni hekima na upeo wa kuyachambua masuala makubwa katika jamii. Falsafa mbalimbali zilichangia kwa kiasi kikubwa kuweko na mabadiliko katika maisha ya wanadamu.

                Maisha na hata kifo cha mwanafalsafa Socrates yalikuwa ni ya ajabu. Aliishi kama mwanafalsafa akiwa kama dira ya jamii na alitakiwa apembenue kila jambo alilonena na mwishoni alitakiwa kunjwa sumu ili ahakikishe kuwa haitamuua na akafa! 

                Afrika haikuwa nyuma katika matukio ya kishujaa. Katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara ambako dola ya Kizulu nchini Afrika ya Kusini ilikuwa na michezo yao iliyoonyesha ujasiri mkubwa wa mashujaa wa kivita. Chini ya utawala wa mfalme Chaka vijana wengi wa jika la kupigana vita walitakiwa kuonyesha ujasiri wao katika mikusanyiko mikubwa ikiwa ni pamoja na michezo iliyowaandaa kuingia vitani. 

                  Ujio wa wazungu katika ukanda huu haukuwa wa kirahisi kabisa kwani walipambana na wenyeji ambao ni Wazulu walishirikiana na makabila mengine shujaa kwelikweli. Hapa Tanzania nako makakabila kama Wahehe, Wangoni, Wasambaa, Wachagga nayo yalikuwa na ujasiri wa kipekee katika kujilinda na maadui zao ikiwa ni pamoja na uvamizi wa wakoloni wa kizungu.  

                 Pengine kwa namna moja matukio yote haya na mengine mengi yana mchango mkubwa sana katika mchezo wa ngumi. Japokuwa mabadiliko ya mchezo huu yametokea sehemu mbalimbali duniani kwa njia moja au nyingine yamekuwa na lengo moja tu nalo ni kujenga ujasiri wa wanadamu. 

                Mtu anapopigana ngumi na kushinda anapendwa na kila mtu. Ni shujaa wa kila mtu. Ni mfano wa kuigwa kwa wale wanaopenda mashujaa. Wanadamu wana asili ya kupenda mashujaa. Hata kama mashujaa hao wana kasoro fulani za kimaumbile lakini wanatukuzwa na kuheshimika kwa ushujaa wao.


Mashujaa daima ni watu ambao jamii inawaona kama kioo chake na mfano wake wa kuigwa. Ili mtu au bondia awe shujaa kwelikweli hana budi kufuata yafuatayo:

1) Awe ni mtu anayefanya vizuri kuliko wote

2) Awe ni mtu anayeishi maisha yasiyo na kasheshe
3) Awe ni mtu aliyefikia kiwango cha juu katika fani yake na kuitetea bila ya matatizo.
4)Na zaidi ya yote awe mtu anayependa nchi yake na kuitetea katika fani yake bila kujali faida anayoweza kuipata.


              Mara nyingi katika fani ya ngumi kumetokea mashujaa wengi waliodumu kwa muda mfupi na hivyo jamii kuwasahau kabisa. Katika nchi za wenzetu kuna utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu za kazi / michango inayotolewa na kila mtu katika fani mbalimbali. Zipo website (tovuti) mbalimbali ambazo ukimtafuta mtu katika fani hizi utapata mara moja. Iaendelea………………………….! 

Mwandishi wa makala haya ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) E-mail:ibfafrica@yahoo.com                                                                                

Comments