Skip to main content

BFT NA TPBC ZAUNDA 'KAMATI YA NYERERE'




Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC} zimekubaliana kuunda Kamati ya watu kumi (lO) ili kufufua na kuundeleza mchezo wa ngumTanzania. 


Kamati hiyo ambayo itajumuisha wajumbe watano (5) kutoka BFT na watano (5) kutoka TPBC itakuwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa TPBC, Godfrey Madaraka Nyerere na itaiwa"Kamati ya Nyerere ya Kufufua nKuendeleza Ngumi Nchini" 

"Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini"  itafanya kazi ya kuandika hadidu rejea za rasimu ya makubaliano ya pande zote mbili ili ziweze kutumika kama mwongozo wa makubaliano hayo. 

Ushirikiano kati ya BFT na TPBC utaratibiwa na Katibu Mkuu wa BFT  Makore Mashaga pamoja na Katibu Mkuu wa TPBC Nemes Kavishe

Wawili hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya "Kamati yNyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini" ambacho ndicho chombo cha kusimamia na kuratibu makubaliano haya. 


Ushirikiano kati ya vyama hivi viwili ambavyo kimoja kipo kwenye ngumi zaridhaa na kingine kipo kwenye ngumi za kulipwa ni ushirikiano unaolenga kubadili mwelekeo wa mchezo wa ngumTanzania. 

Kwa muda mrefu sasa mchezo wa ngumi umekuwa ukikumbwa na matatizo mbalimbali ambayo yamepelekea kutokuwepo na maendeleo yanayotegemewa na wadau wa ngumi Tanzania. 

Ushirikiano wa vyombo vyote vinavyoratibu ngumi hapa Tanzania utakuwa ni msingi imara wa kujenga ari ya maendeleo ya ngumi hapa Tanzania. 
Tanzania imekuwa ikivurunda kwenye mashindano ya kimataifa karibu kila mchezo hivyo ushirikiano wa vyombo hivi viwili vya ngumi utakuwa ndio msingi imara wa kuendeleza mchezo huo Tanzania .

Imetolewa kwa pamoja na:



)1(~~",



Makore Mashaga

Katibu Mkuu 
BFT 

Onesmo Ngowi
Rais 
TPBC

                                            

Comments