FFU ! NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA AFRIKA-MESSE,BREMEN 15.09.2012


                                                 Kamanda Ras Makunja
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU,yenye maskani yake kule Ujerumani,bendi hiyo inayokamatia taji la kimataifa la
"IDA-International Diaspora Award' inatarajiwa kutumbuiza katika maonyesho mengine makubwa siku ya jumatano 12.09.2012 itakua mjini Bremerhaven, na Jumamosi ya 15.9.2012 Kikosi kazi hiko kitapeleka nguvu zote katika maonyesho  makubwa ya biashara ya kiafrika "AFRIKA-MESSE" Bremen,yatakayafanyika mjini Bremen,Ujerumani.
Bendi hiyo inayotamba CD mpya "Bongo Tambarare" ambayo imeshatua kwa kishindo katika vituo vya redio mbali mbali ndani na nje.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 muhasisi wake Kamanda Ras Makunja,
 wa FFU,ambaye pia ndiye kiongozi wa kikosi kazi hiko.
Kikosi kazi hiko kilichojizolea washabiki kila kona duniani kimekua tishio la kimataifa,inasemekana kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyo fanikiwa kuteka nyoyo za washabiki wa kimataifa na kuwafanya washabiki kuwa ndio wamiliki wa bendi hiyo.
Usikose kuwasikiliza bofya at www.ngoma-africa.com