BWANA ALLEN MUNENE NA BI VERONICA STIMA WAMEREMETA HUKO TABORA

 Padre Kalaso (kati) wa Kanisa la Familia Takatifu Parokia ya Ipuli, Tabora akishuhudia Bwana Allen Munene akimvalisha pete bibi Veronica Stima wakati wakifunga ndoa takatifu iliyofanyikia kanisani hapo na kufuatiwa na sherehe iliyofayika katika ukumbi wa chuo cha Utumishi wa Umma Uhazili, Tabora.
Bibi Veronica Stima akimvalisha mumewe Allen.
Wakiwa katika nyuso za tabasamu zito ni Bwana na Bibi Allen Munene.
Padre Kalaso (kati) wa Kanisa la Familia Takatifu Parokia ya Ipuli, Tabora akimuelekeza Bwana Allen Munene kutia saini katika cheti huku pembeni yake mkewe Veronica akishudia.
Nae mkewe akitia saini.
Wakiwa katika nyuso za furaha na kuonyesha vyeti vyao.
Pongezi nyingi zikiwamiminikia Bwana na Bibi Allen mara baada ya kufunga pingu za maisha.
Mama mzazi wa Bibi harusi akitoa baraka zake za pekee kwa mwanae mpya wa kiume ambaye ameungana na mwanae.
Pozi la pekee; bibi harusi akiwa na wasimamizi wake.
 ...Maharusi wakiingia ukumbini kwa furaha.

 
...wakishangiliwa mara baada ya kukata utepe na kuingia ndani ya ukumbi.
...wapambe nao wakiingia kwa madaha.
Bibi Veronica akigawa shampeni kwa wakwe zake.
 Nae bwana Allen Munene akigawa shampeni upande wa wakwe zake.
 ...Tunywe kwa afya na maisha yetu...
Wapendanao wakikata keki kuonyesha umoja na upendo kati yao.
 Maharusi wakigawa keki upande wa Mzee Munene.
 ...Huku nako Baba na Mama Stima wakipokea keki kutoka kwa watoto wao.
 ...nderemo na vifijo vilitawala ukumbini...
 Wachanga na ile staili yao ya kushikana mikono, kudumisha umoja na mshikamano kati yao.
 ... Upendo na mshikamano udumu milele.
 Wapare nao hawakuwa nyuma na staili yao ile ya kuwema mikono nyuma...
 Wafipa sasa wao walikuja kisasa kabisa...
 ...huku nako mambo ya pwani yaliendelea kunoga...
 ... Ni bwana Cathbert Angelo mmiliki wa mtandao huu nikiwa na mama na baba zako (wakwe). Mavazi ya Bwana na Bibi Allen Munene yamebuniwa mbunifu wa mavazi Manju Msita.