YONDAN, REDONDO KUJADILIWA J'2


Yondan
Redondo

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
Usajili utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
 Ndani ya kikao hicho moja ya jambo litakalochukua nafasi ni kuhusiana na usajili wa wachezaji Ramadhan Chombo 'Redondo' aliyesajiliwa Simba kutoka Azam Fc ambayo inadai mchezaji huyo bado ana mkataba, Kelvin Yondan ambaye amesajiliwa na Yanga na kutoka Simba huku Simba nao wakiwakilisha jina lake.