YANGA YAUA TENA KIGALI

MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga SC ya Dar es Salaam, leo wamekamilisha ziara yao nchini Rwanda, kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Amahoro.
Stefano Mwasyika aliisawazishia Yanga, baada ya Fabrice kutangulia kuifungia Polisi na Nahodha Msaidizi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akafunga la pili.
Katika mchezo wa awali juzi, Yanga waliichapa Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja huo huo wa Amahoro mjini Kigali.
Yanga inatarajiwa kurejea kesho Dar es Salaam.

Yanga SC. Habari picha kwa hisani ya bongostaz.blogspot.com