YANGA WATEMBELEA MAKABURI YA KIMBARI, KUIVAA RAYON IJUMAA

MABINGWA wa KAgame Yanga, mchana wa leo walitembelea makaburi ambayo walizikwa wahanga wa mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Yanga ipo nchi humo kwa mwaliko wa Rais wa huko Paul Kagame aliyewaita kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na kutwaa ubingwa wa Kagame katika michuano iliyofanyika nchini mwezi uliopita.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Abdallah Binkleb aliimbia Dina Ismail Blog kwamba  baada ya ziara hiyo, jioni wachezaji wa timu hiyo walifanya mazoezi katika uwanja wa Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA).
Binkleb ameongeza kwamba, kesho watakwenda Ikulu kutimiza mwaliko wa Rais Kagame kabl ya Ijumaa kucheza na Rayon na mchezo mwingine utakuwa Jumapili dhidi ya Polisi ya huko