YANGA WAREJEA KUTOKA MJENGONI, KUENDELEA NA KAZI KESHO

Mabingwa wa Kombe la Kagame, Klabu ya Yanga imerejea jijini Dar es Salaam mchana wa leo kutoka mkoani Dodoma ilipokwenda huko kwa ajili ya ku[pongezwa na wabunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu wa Yanga, Mwesiga Selestine amesema leo kwamba baada ya mapumziko ya jioni ya leo kikosi hicho kesho kitarejea katika viwanja vya sekondari ya Loyola kuendelea na mazoezi yake ya kawaida kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali.