YANGA KUANZA KUJIFUA KESHO

Tom Saintfiet, kocha wa Yanga
MABINGWA wa Kagame Yanga kesho wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na michuano mbalimbali.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba wachezaji wa kikosi hicho waliotoka nje ya jiji la Dar es Salam wameshawasili tayari kuanza mazoezi yatakayofanyika uwanja wa Shule ya sekondari Loyola jijini Dar es Salaam chini ya kocha mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet.