'YANGA KAMA MNAMTAKA OKWI LETENI DOLA MIL.2'

WAKATI mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi akifuzu majaribio yake katika klabu Red Bulls Salzburg  ya Austria, uongozi wa klabu ya Simba umewataka masimu wao wa jadi nchini Yanga kutoa dola za kimarekani Mil.2 iwapo wanamtaka Okwi.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alipozungumxza katika mkutano wa wanachama wa Simba uliofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oyesterbay jijini Dar es Salaam.