VODACOM KUENDELEA KUDHAMINI LIGI KUU BARA


KAMPUNI ya Vodacom Tanzania inatarajia kuendelea kudhamini ligi kuu soka Tanzania BAra inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba Mosi, imefahamika.
Awali kuliwa na taarifa kwamba kampuni moja ya bia nchini ilikuwa na mpango wa kudhamini ligi hiyo, lakini Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania  (TFF), Angetile Osiah alisema jana kwamba mazungumzo baina yao na mabosi wa Vodacom yapo katika hatua za mwisho.
Mkataba wa Vodacom na TFF, unafika tamati Septemba mwaka huu ambapo tangu walipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2007 ambapo udhamini huo, wametumia zaidi ya sh bilioni 1.3 kwa ligi nzima.