VILABU VYATAKIWA KUWASILISHA HATI ZA VIPIMO VYA AFYA (MEDICAL TEST) VYA WACHEZAJI

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)limezitaka klabu  zote zilizowasilisha  maombi ya usajili kwa wachezaji wao kuwasilisha na nakala za hati za vipimo vya afya (medical certificate).
Ofisa habari wa TFf, Boniface Wambura amesema kwamba zoezi hilo ni  kwa mujibu wa kanuni za usajili za shirikisho hilo.