UBINGWA WA YANGA WAMFUKUZISHA KAZI KOCHA


SIKU chache baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame klabu ya soka ya Azam Fc imemtimua kocha wake mkuu Muingereza Stewart Halll, imefahamika. 
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kwamba sababu ya kumtimua kocha huyo ni kitendo cha kumpanga nyota wa timu hiyo Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali ya Kombe la Kagame baina ya Azam na Yanga ambapo Yanga ilitwaa ubingwa  baada ya kuifunga Azam mabao 2-0.
Inaelezwa kuwa uongozi ulikerwa na kitendo cha Ngassa ambaye kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kuwa na ‘Uyanga’ na hivyo kocha kumuweka benchi katika mechi za kombe la Kagame, alipoibusu na kuvaa jezi ya Yanga baada ya mchezo baina ya Azam na Vita.