TWITE KUTAMBULISHWA UWANJA WA TAIFA KESHO

MABINGWA wa kombe la Kagame Yanga kesho watamtambulisha rasmi beki wao wa kimataifa Mbuyu Twite kupitia mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Coastal Union ya Tanga utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Twite ambaye alizua gumzo baada ya kujisajili Simba na baadaye Yanga ambao walimpandishia dau aliwasili jana na leo alianza mazoezi na wenzake katika uwanja wa Loyola.
Msemaji wa Yanga Lous Sendeu amesema kwamba pamoja na Twite, mashabiki wa Yanga watapata kuwaona nyota wengine wapya waliosajuiliwa katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa ligi na michuano mbalimbali.
Alisema viingilio katika m,chezo ni sh 20,000,10,000, 5,000 na 3000.