YANGA KUPELEKA KOMBE LA KAGAME BUNGENI


MABINGWA wa soka wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ Yanga kesho wataondoka jijini Dar es Sala kuelekea Dodoma kw ajili ya kwenda kupongezwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu mesema zoezi la utambulisho linatarajiwa kunayika jumatatu  mchana baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge cha asubuhi. 
Alisema mbali na wachezaji hao kutambuylishwa na kupongezwa bungeni, pia watatumia ziara hiyo kufungua tawi maalum la Yanga.