SIMBA WAENDA A-TOWN, KUKIPIGA NA AFC LEOPARDS


MABINGWA wa ligi kuu soka Tanxzania Bara, Simba wanaondoka leo kwenda jijini Arusha kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba timu hiyo itarejea jijini wsiku moja kabla ya mchezo wao wa kuwania Ngao ya Jamii baina ya Azam Fc.
Aidha ikiwa mjini Arusha, inatarajiwa kukipiga na AFC Leopards ya Kenya mchezo utakaopigwa Agosti 18 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo.