SIMBA SC YAMUACHA MRWANDA

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sc ambao wametua jana mjini Arusha kwa ajili ya kambi maalum ya ligi kuu soka Tanzania Bara na mkichezo mingine, wamemuacha mshambuliaji wao Danny Mrwanda katika safari hiyo.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba Mrwanda ameachwa kutokana na kuwa katika maandalizi ya ndoa yake.