SIMBA KUPEPETANA NA AFC LEOPARDS J'2

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba,  Jumapili watashuka katika simba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kuvaana na AFC Leopards ya Kenya.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba mchezo huo ni maalum kwa kujua kuipa makali timu hiyo ambayo ipo katika maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania Bara.
Alisema kikosi cha Simba kilichopiga kambi mjini humo kinaendelea vema na maandalizi yake.