SIMBA KUKIPIGA NA NAIROBI CITY STARS J'2TIMU ya Simba inatarajia kucheza mechi dhidi ya timu ya soka ya NAIROBI CITY STARS siku ya Jumapili ijayo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.
Timu hiyo kutoka Kenya ndiyo iliyocheza na Simba jijini Dar es Salaam katika tamasha la Simba Day.
Awali Simba ilikuwa imepanga kucheza mjini Tanga WIKIENDI HII lakini kutokana na mabadiliko ya programu ya mazoezi ya benchi la Ufundi, Wekundu wa Msimbazi sasa watabaki Arusha hadi Septemba nne mwaka huu ili kukamilisha programu yote bila ya usumbufu.
Hali ya kikosi cha Simba ni ya utulivu kabisa na mazoezi yanafanyika kwa mchanganyiko wa mazoezi ya uwanjani na GYM.
Hakuna majeruhi yoyote hadi sasa na wachezaji wote wanafanya mazoezi kama kawaida.