SIMBA KUKIPIGA NA CITY STARS YA KENYA KESHOKUTWA

Geofrey Nyange 'Kaburu', Makamu Mwenyekiti wa Simba


MABINGWA wa ligi Kuu bara Simba jumatano ya keshokutwa watacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na timu ya City Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, katika mchezo maalum ya maadhimisho ya tamasha la Simba Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema leo kwamba mbali na mechi hiyo pia watatambulisha nyota wake wapya iliyiowasajili kutoka timu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Aidha, tamasha hilo ambalo litambwa na burudani mbalim,bali litatumika pia kuwatunuku wadau mbalimbali waliochangia kwa mafanikio ya Simba kwa namna moja ama nyingine.
"Pia kutakuwa na tuzo maalum kwa mchezaji bora wa msimu uliopita wa Ligi, pia mchezaji mwenye nidhamu tutamzawadia tuzo,"alisema