SIMBA B' KUSHIRIKI MICHUANO YA SUPER 8

TIMU ya Vijana ya Simba ndiyo itakayoshiriki katika michuano maalum ya Banc ABC Super 8 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 4 hadi 18 kwa kushirikisha timu nane kutoka Tanzania bara na Visiwani.
Simba imaemua kuipeleka timu ya vija na kutokana na timu ya wakubwa kuwa katika programu nyingine kwa kipindi hicho.
Hata hivyo taarifa hizo ni taarifa za wali lakini huernda mambo yakabadilika baada ya viongozi wa Simba kukutana na TFF pamoja na waandaaji wa michuanio hiyo kuzungumzia mustakabali mzima wa michuano hiyo yenye lengo la kuzinoa timu hizo kabla ya kuyshiriki katika ligi kuu bara.
Banc ABC imeingia mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya kudhamini michuano hiyo itakayiokuwa ikipigwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid-Arusha, CCM Kirumba-Mwanza, Taifa-Dar es Salaam na Amaan -Zanzibar.